HISTORIA FUPI YA UGONJWA WA CORONA 

Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu.. Kwa binadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji.  Maradhi yaliyowahi kusababisha madhara makubwa kutokana na virusi vya Corona ni pamoja na MERS na SARS yaliyozuka mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kirusi cha Corona kilichogundulika hivi karibuni kinasababisha ugonjwa unaofahamika kama COVID-19.
COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019. Hadi sasa virusi hivi vimeenea duniani kote na vimekuwa tishio kubwa duniani
DALILI ZA VIRUSI VYA CORONA. 


Zipo dalili mbali mbali za ugonjwa huu kama zilivyo orodheshwa hapa chini. Dalili kuu za Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu na zinatokea taratibu. Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi. Lakini isikutishe, ni mtu 1 pekee kati ya watu 6 walioambukizwa virusi vya Corona hufikia dalili hiyo ya hatari. Na asilimia 80 ya walio na virusi hivyo hupata nafuu bila kuhitaji msaada wa matibabu.

MAKUNDI YALIO KATIKA HATARI YA KUATHIRIKA ZAIDI NA UGONJWA  HUU. 

WHO inasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu kama Shinikizo la Damu, Kisukari, Matatizo ya Figo ndiyo walio kwenye hatari zaidi ya kuathika pindi wanapopatwa na virusi vya Corona. Watu wa umri wa wastani na wenye afya imara wanaweza kupata virusi vya Corona na kupona bila kuhitaji matibabu.

JINSI YA VIRUSI VYA CORONA VINAVYO SAMBAA
Watu wanaweza kupata Virusi vya Corona kutoka kwa watu walioambukizwa. Virusi vinaweza kusambaa kupitia maji maji kutoka kwenye pua au mdomo wa aliyeathirika. Iwapo mtu anagusa maji maji kama mafua, mate na makohozi ya mtu aliye na virusi na kisha kujigusa mdomo, macho na pua anaweza kupata virusi vya Corona.

NAMNA YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA '


Nawa vizuri na kila wakati mikono yako kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu kwa angalau sekunde 20.Kaa umbali wa angalau hatua mbili (2) kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi.Hakikisha wewe, na walio karibu yako wanazingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya.Baki nyumbani ikiwa hujisikii vizuri. Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kwa sababu huko wataalamu watakupatia msaada muhimuEpuka kuwa sehemu yenye msongamano, kama vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye yenye mgandamizo wa hewa.Nunua kifunika mdomo na pua na kukikavaa ukiwa kwenye mikusanyiko.Fuatilia taarifa za afya na matangazo yake kuhusu virusi vya Corona.


NINI TIBA YA CORONA. 

Hadi sasa hakuna tiba au chanjo dhidi ya virusi vya Corona lakini kwa sababu virusi hivyo vinaleta dalili mfano wa zile za mafua makali, mchanganyiko wa tiba unatumika kupunguza athari za virusi vya Corona.

MADHARA YA UGONJWA HUU. 
Hakika kila mtu anakubaliana na jambo hili ya kwamba ugonjwa huu wa corona umeleta madhara makubwa. Madhara hayo ni kama yafuatayo. 
. Kusababisha vifo
. Kuyumba kwa uchumi
. Shughul I Nyingi duniani kusitishwa kama michezo, shule, usafiri wa anga pamoja na majini. 
. Watu kutoruhusiwa kutoka nje kwa baadhi ya mataifa 
. Kusababisha ofu kubwa kwa watu

FAIDA 
  • Kuongeza ajira katika sector ya afya
  • Kutoa furusa za wanasayansi kufanya utafiti juu ya ugonjwa huu
  • Kuwapa furusa ya ubunifu makampuni yanayo zalisha vifaa vya kujikinga. 

Tuendelee kufatilia zaidi. Katika blog yako pendwa ya DIDAS BLOG NEWS 



Keep your environment safe and I love Tanzania