Wapendwa leo tutaangalia kidogo upande tofauti, naule tuliozoea, leo tuko upande wa mazingira, kwani endapo tutayaboresha basi na shughuli zetu za kiujasiriamali zitaweza kufanyika vizuri sana, karibu sasa twende pamoja.
Mazingira
ni mambo yote yanayo athiri ukuaji au uwepo wa viumbe hai,mfano hewa,maji na
ardhi.Mazingira ni kitu muhimu sana katika ustawi wa viumbe hai wowote,katika
dunia hii tuliyomo.Mazingira ni muhimu kwa ukuwaji ya mimea mbalimbali,viumbe
wabaharini,viumbe walioko chiniya ardhi,na viumbe walioko juu ya uso wa dunia.
Sera
mbalimbali za uifadhi wamazingira na viumbe vyake zimewekwa kwa lengo mmoja
kubwa kwanza kutunza mazingira lakini pili kulinda aina ya viumbe
waliomo(species).Mfano sera ya mazingira ya mwaka 1997 ina tamka wazi na
inazitaka wizara zote namtu mmoja mmoja kuweka au kuchanganya swala la mazingira
katika miradi yao au katika shughuli zao,yani lazima kuwe na ‘equal balance’maendeleo katika shughuli
zao lakini na hakikisho la kuweka
mazingira endelevu kwa ajili ya maisha yaviumbe hai.
Sera
yaelimu na mafunzo ya mwaka 1996, inazitaka taasisi zote za elimu kuongeza
uelewa wa maswala yamazingira kwalengo la kuendelezaupatikanaji wa taarifa linapokuja
suala la kufanya maamuzi kwenye jambo la mazingira.
Pia
kwenye suala la kulinda viumbe hai mfano nyuki, sera inasema hivi, “any
investment that takes place inside or around bee reserves and apiaries don’t
pose potential damage or danger to bees,bee products and bee fodder plants”.Tafsiri
isiyo rasmi ni kwamba, uwekezaji wowote unao fanyika ndani au eneo la hifadhi
ya nyuki na kwenyemizinga yao, usiharibu au kuhatarisha nyuki pamoja na malisho
yao.
Kwa
hiyo kwa na mnamoja au nyingine tuna ona umuhimu wa kutunza mazingira kwa faida
yetu na viumbe hai vinavyo tuzunguka kwakuwa sisi soteni mazingira na mazingira
ni sisi.
Faida
ya moja kwa moja tunayo pata kwa kutunza mazingira vizuri ni kuongeza umri wa kuishi
katika ulimwengu huu tulionao na kuishi kwa raha mstarehe.
Maisha
yetu yamekuwa mafupi kwa sababu tumearibu mazingira. Kunauhusiano mkubwa kati
ya umri wa maisha yetu na uhifadhi wa
mazingira,maisha yetu yanakuwa mafupi kwa sababu tuna kula vitu visivyo na
ubora na ambavyo avijengi mwili bali kuharibu mwili, na vyakula hivyo havina
ubora kwa kuwa ardhi inayotoa hayo mazao imeharibiwa na shughuli za binadamu.
Kwa hiyo ardhi haina rutuba, yaasili, ina bidi tuweke mbolea za viwandani ili
angalau kuifanya au kuirudishia tena rutuba kama ile ya mwanzo, ili ituletee
mazao bora kwa ajili ya afya zetu, kitu ambacho ni kigumu sana, kurudisha
ualisia wa awali.
Jambo
linguine kubwa tunalo nufaika nalo endapo tutajitaidi kutunza mazingira, ni hakikisho la
viumbe hai vyote kwa maana mazao yamisitu na wanyama ambayo kwayo, uwepo wake
una tufanya tutegemeane wote, yani miti na viumbe wengine wanatutegemea
binadamu katika kuendelea kuwepo, na sisi tuna vitegemea viumbe hivi ili
tuendelee kuwepo.
Kwa
hiyo ni muhimu kujitaiditi kutunza mazingira kwa faida yangu nayako.
Nini
cha kufanya kwa wale ambao ili maisha yao yaende kilasiku inabidi waaribu mazingira? Kuna njia angalau za
kufanya ili kupunguza uharibifu wa mazingira, mmoja wapo ni kufanya/kugeuza au
kudurufu takataka na kuwa malighafi tena kwa ajili ya kutumia(recycle), mfano
karatasi zisizotumika zinaweza kulowekwa kwenye maji alafu zikikaushwa zina
weza kutumika kama mkaa, maji machafu yanaweza kugeuzwa kuwa maji safi tena,
ingawa ukweli baadhi yahizi njia zinaitaji utaalamu kidogo, lakini kama una nia
utafanikiwa, jaribu kuwaona watukama SIDO,TATEDO,wanaweza
kukupa msaadazaidi nini cha kufanya ili kufikia kufanya mapinduzi ya kijani.
Maranda
ya mbao yana wezakugeuzwa na kuwa bidhaa bora ya kupikia ikawa badalaya kukata
kata kuni ovyo. Mbolea ya wanyama kama ngo’mbe ukipata utaalamu kidogo kwa watu
nilio kwa mbia ina weza kukusaidia kupata nishati nzuriya kupikia ikawa ni
mmbadalawa kuni, hata uchafu wa jikoni
kama maganda ya vitunguu, nyanya mabaki ya vyakula kwa namna moja au
njingine vina weza kubadilishwana kuwa nishati, kuna watu wanautaalamu wa
kufanya shughuli hizi kwa mfano Dr.Didas wa MJASIRIAMALI KWANZA, wanaweza
kukupa utaalamu huu, na wewe ukaishi kwa raha mstarehe.
0 Comments