MWANAMKE WA KWANZA TZ KUWA RAISI

MWANAMKE WA KWANZA TZ KUWA RAISI

Kutokana na majonzi makubwa ya kumpoteza kiongozi mkubwa nchini Tanzania yaani Risi wetu mtukufu marehemu ,mh dr. john pombe magufuri alie aga dunia siku ya tarehe 16/03/2021. ukweli kila mtanzania amepokea taharifa hizi kwa mstuko na masikitiko saana, bwana ametwaa jina lake liimidiwew.


kutokana na msiba ulio ikumba nchi yetu ya Tanzania na kwa mjibu wa katiba ya Tanzania ni wazi kwamba makamu mmkuu wa Tanzania atakaimu kiti cha raisi kwa mda ulio bakia hvyo  ni historia kubwa sasa Tanzania kuwa nayo ya makamu mkuu kukaimu kiti cha raisi.
nimtakie majuku mema na tuzidumishe itikadi za mh marehemu raisi wetu alizo kuwa naozo ili tuweze kusonga mbele kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni pia.
hvyo bas mjue kwa undani makamu wa raisi ya Tanzania ambaye anatarajia kuapishwa rasimi siku za hivi karibuni kuwa raisi wa tz.

id="google_ads_iframe_/4817/bbcworldservice.live.site.swahili/swahili_habari_content_0__container__" style="border-image: none; border: 0pt;">

Kifo cha Magufuli: Mfahamu Samia Suluhu Hassan, Rais ajaye wa Tanzania

Samia Hassan

Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa atakuwa mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki jana Jumatano Machi 17.

Samia atashikilia wadhifa huo kwa kipindi kilichosalia cha cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

Anatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu zaidi nchini Tanzania. Pia atakuwa rais wa pili wa Tanzania kutokea Zanzibar, wa kwanza akiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 10 kutoka mwaka 1985 mpaka 1995.

Hii pia ni mara ya kwanza kwa nchi ya Tanzania kufiwa na rais akiwa madarakani na makamu wake kuchukua nafasi.

Lakini je, Mama Samia ni nani?

TWITTER/@SULUHUSAMIA

Chanzo cha picha, TWITTER/@SULUHUSAMIA

Kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, msafara wa aliyekuwa mgombea mwenza wa CCM, Samia Hassan Suluhu, ulikuwa na wasanii wengi mashuhuri nchini.

Awali, wengi walimwogopa kwa sababu ya heshima yao kwake - lakini kuvunja mipaka, akaomba jambo moja kwao; wamwite Mama.

Tangu hapo, ukuta kati yao ukavunjika na kampeni zake zikawa na msisimko na hamasa kubwa - tofauti na ilivyozoeleka kwenye matukio ya wagombea wenza.

Kwa Watanzania wengi, jina la Samia Hassan Suluhu (60) lilipata umaarufu zaidi wakati alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba lililoteuliwa mwaka 2014.

Tanzania ilikuwa inaelekea kutengeneza Katiba mpya - baada ya kukamilika kwa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kupitia Tume ya Jaji Warioba na Mama Samia alikuwa amepewa jukumu la kuongoza mchakato huo kupitia Bunge la Katiba.

Kwa sababu bunge lile lilikuwa likionyeshwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya runinga na Watanzania wengi wakiwa na kiu kubwa ya kujua nini kinaendelea - sura ya Samia ilianza kuzoeleka kwenye macho ya wengi na uwezo wa kuongoza ukionekana dhahiri.

TWITTER/@SULUHUSAMIA

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini hiyo ilikuwa taswira yake ya hadharani. Katika duru za kisiasa bungeni wakati ule, Samia alikuwa akifahamika kwa uwezo wa kuonyesha utulivu - hata katika nyakati ambazo hali ya hewa katika bunge hilo ikiwa imechafuka na pia kuzungumza na wote.

Muundo wa bunge hilo ulitaka viongozi wake wa juu watoke katika pande mbili za muungano na kwa vile mwenyekiti wa bunge hilo alikuwa ni hayati Samuel Sitta kutoka Tanzania Bara, nafasi ya Makamu Mwenyekiti iliangukia kwa Mzanzibari Samia.

Hata hivyo, wengi hawakutarajia kwamba angetangazwa na aliyekuwa mgombea urais wa chama cha mapinduzi mwaka 2015, John Magufuli, kuwa mgombea mwenza wake kwenye uchaguzi huo.

Ingawa wakati huo tayari alikuwa na uzoefu wa uwaziri wa takribani miaka 15; kujumlisha na uzoefu wake huo katika Bunge la Katiba- si watu wengi walimwona yeye kama mmoja wa watu wanaoweza kupewa wadhifa huo.

Wakati CCM iliposhinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 - unaotajwa kuwa mgumu kuliko yote kwa chama hicho tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini - Samia aliweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo tangu kuanzishwa kwa taifa la Tanzania.

Siri ya mafanikio ya Samia

Samia Hassan Suluhu

Sifa moja kubwa ambayo watu waliowahi kufanya naye kazi wanaisema na ambayo si watu wengi wa nje wanaifahamu ni uwezo wake mkubwa wa kiuongozi.

Mbunge wa jimbo la Bumbuli (CCM), January Makamba, anasema Samia ni miongoni mwa wanasiasa wenye uwezo mkubwa aliowahi kufanya kazi nao na ni bahati mbaya tu kwamba wengi wa Watanzania hawajapata fursa ya kuliona hilo.

Makamba alifanya kazi kwa karibu na mama samia katika kipindi cha kati ya mwaka 2015 hadi 2020 wakati akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - ambapo alikuwa akiripoti kwa mama huyo moja kwa moja.

"Mama Samia amedunishwa. Ana uwezo mkubwa wa kufanya aonekane ni mwanasiasa wa kawaida lakini ukweli ni kwamba uwezo wake ni mkubwa sana na hili sijasimuliwa na mtu bali nimeliona kwa kufanya naye kazi kwa karibu," alisema.

Maelezo ya video,

Samia Suluhu Hassan: Fahamu maisha na majukumu ya makamu wa rais wa Tanzania

Mama Samia anaelezwa kama mwanasiasa anayependa kufanya maamuzi kupitia kusikiliza kila mmoja na si mtu wa kuamua mambo kwa pupa au kwa kuonea wengine.

Samia pia anaelezwa kuwa mwanasiasa jasiri na asiyeyumbishwa kwenye jambo analoliamini na kulikuwa na maneno kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM kumfanya yeye kuwa mgombea mwenza wa Magufuli kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kulitokana pia na kufahamu sifa yake hiyo.

Kwa vile Magufuli ni mtu anayeamini katika kusukuma mambo kwa haraka na wakati mwingine bila kujali athari za kisiasa au kisaikolojia kwa uamuzi huo, CCM ilitaka Makamu atakayekuwa na uwezo wa kumwambia ukweli bila kumwogopa badala ya kukubali kila kitu.

Mfano mmoja wa tabia za Samia ni kitendo chake cha kwenda kumjulia hali aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alipokuwa amelazwa nchini kenya.

Katika mojawapo ya matukio ya kutisha kwenye historia ya Tanzania, Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba mwaka 2017 akiwa jijini Dodoma alikokuwa anahudhuria vikao vya bunge.

Samia alikuwa ndiye kiongozi wa juu wa kwanza wa serikali - na pekee, kwenda kumuona mwanasiasa huyo mashuhuri.

Historia ya Samia kwa ufupi

Samia Hassan Suluhu

Mama Samia aliolewa na mumewe, Hafidh Ameir, mnamo mwaka 1978 na katika ndoa yao wamejaliwa kupata watoto wanne.

Mtoto wake maarufu zaidi - Wanu, ni mbunge wa bunge Tanzania.

Samia ni msomi wa kiwango cha shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza na ni mhitimu pia wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alikosomea masuala ya utawala.

Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar mwaka 1977 na akapanda ngazi hadi kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988.

Alihudumu pia kama meneja wa mradi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Zanzibar kati ya 1985 na 1997, na pia kama meneja mkurugenzi wa Mwamvuli wa NGO 1998 hadi 1999.

Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa.

''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija. Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii


Post a Comment

0 Comments