Kusikiliza TANZANIA EU SIASA JOHN POMBE MAGUFULI CHADEMA Imechapishwa 24-02-2018 • Imehaririwa 24-02-2018 Saa 15:08 Umoja wa Ulaya wasikitishwa mauaji yanayokea Tanzania na RFI Bendera ya Umoja wa Ulaya REUTERS/Toby Melville Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko la kuelezea wasiwasi wake kuhusu matukio ya mauaji yanayotokea nchini Tanzania na ambayo yanatishia haki za kidemokrasia. Tamko hilo la Umoja wa Ulaya limetolewa kwa ushirikiano na mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na kuungwa mkono na mwakilishi na mabalozi wa Norway, Kanada na Uswisi. “Tunashuhudia kwa wasiwasi mwendelezo wa matukio ya hivi karibuni yanayotishia nidhamu ya demokrasia na haki za watanzania, katika nchi iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa utulivu, uhuru na amani,”imesema sehemu ya taarifa hiyo. Umoja huo umetaja tukio la karibuni la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Akwilini Akwiline Bafta na kusema unakaribisha wito wa rais wa Tanzania John Magufuli wa uchunguzi wa haraka. Akwilina Akwiline Bafta alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na aliuawa kwa kupigwa risasi wakati polisi ikitawanya maandamano ya Chama Kikuu cha Upinzani, Chadema. Alizikwa jana wilayani Rombo, Mkoani Kilimanjaro. Aidha, Umoja wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la ripoti za ukatili katika miezi ya karibuni ambapo mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasijulikana na kutoweka kwa mwandishi wa habari wa habari wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda Matukio mengine yaliyotajwa kwenye taarifa hiyo ni mashambulio yaliyopelekea kupoteza uhai kwa serikali, wawakilishi wa vyombo vya usalama na wananchi yaliyotokea Mkoa wa Pwani ndani ya miaka miaka miwili iliyopita. Ripoti ya Mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka .mambo haya yafanyiwe kazi sio mzaa.
DIDAS BLOG NEWS IS BEST STATION.