Aliyekuwa Waziri wa nishati na madini prof. Sospeter Muhongo, hajaonekana Bungeni mjini Dodoma bila ruhusa ya Spika tangu uteuzi wake katika baraza la mawaziri utenguliwe wiki tano zilizopita . Mei 24, mwaka huu, Ris John Mgufuli alitengua uteuzi wa prof. Muhongo katika baraza la mawaziri, ikiwa ni muda mfupi baada ya kukabidhiwa ripoti ya kamati ya kwanza ya uchunguzi wa machanga wa dhahabu (makinikia) Mtaalamu huyo wa jiolojia wa kimataifa hakuwapo bungeni wakati uteuzi wake wa uwaziri ukitenguliwa, huku taarifa zikidai kuwa alirudi nyumbani kwao, Musoma Mkoani Mara, kuhudhulia mazishi ya dada yake. Katibu wa bunge DK. Thomas Kashililah, alisema ofisi yake haina taarifa ya mbunge huyo wa Msoma Vijijini (CCM) jambo ambalo ni kinyume na utaratibu. Kiongozi huyo wa bunge pia alisema ofisi yake haijui aliko tangu alipoachishwa nafasi ya uwaziri mwishoni mwa mwezi uliopita DK. Kashililah aliongeza kuwa kwa kawaida mbunge anapokuwa na udhuru , humwandikia Spika kumuelezea hatakuwa bungeni kwa muda Fulani na ofisi ya KAtibu wa Bunge hupewa nakala. “Sijapata nakala yeyote ya udhuru, wa profesa Muhongo na wala sijui alipo tangu siku ile,” alisema DK. Kashililah. Katibu wa Bunge huyo alisema hii ni mara ya pili kwa Muhongo kuondoka Bungeni kwa muda mrefu bila ya ruhusa kwani hata alipomwandikia barua ya kujiuzulu Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, hakuhudhulia bunge kwa muda mrefu. Prof. Muhongo alijiuzulu nafasi ya uwaziri wa Nishati na Madini Januari 24,2015 kwa shinikizo la Bunge, kutokana na taarifa ya kamati moja ya chombo hicho juu ya kashfa ya uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow. Visit DIDAS BLOG NEWS
0 Comments